Kusudi la mwongozo huu ni kutoa habari , taratibu na mwongozo wa shughuli za kuhifadhi kasa wa bahari nchini Kenya. Shughuli za uhamasisho na elimu zinazoelezwa katika mwongozo huu lazima zitekelezwe kwa ushirikiano wa mashirika ya kiserikali ambayo yameruhusiwa kusimamia na kulinda kasa wa bahari. Mwongozo huu utakupatia undani zaidi kuhusu kasa wa bahari na nafasi ya kufanya kazi na watalamu wa kasa na utakupa fursa ya kuhusika kwa ujasiri na shughuli za kuhifadhi kasa. Mwongozo huu ulitayarishwa kwa kuelewa kwamba utaratibu wa elimu na uhamasisho ni muhimu katika kuleta mabadaliko katika mitazamo ya watu na kwa hivyo kusababisha usimamizi wa uhifadhi kwa ushirikiano. Pia hufahamisha vikundi tofauti lengwa kuhusu thamani na kiwango cha matumizi ya asilimali yao. Habari katika mwongozo huu zinaweza kutumiwa kufundisha wanafunzi wa shule, jamii wenyeji ikiwa ni pamoja na wavuvi, vikundi kama akina mama na vijana hata wafanya kazi wa hoteli na wageni.